Msanii wa muziki kutoka Uganda Ziza Bafana ni moja kati ya wasanii tajika nchini humo na amekuwa kwenye muziki kwa miaka kadhaa sasa kabla ya kupotea kwenye game baada ya kubadilisha menejimenti yake iliyokuwa ikisimamia kazi zake.
Kutokana na kutofanya vizuri kwenye muziki Ziza Bafana alihamua kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya ili aweze kusahau masaibu yaliyokuwa yakimsibu.
Sasa akiwa kwenye moja ya interview Mkali huyo wa ngoma ya akalulu amedai kuwa anguko lake kimuziki lilisababishwa na uchawi aliofanyiwa na wasanii wenzake.
Ziza Bafana ameenda mbali zaidi na kusema kwamba wasanii wengi nchini uganda wanatumia nguvu za giza kuwazima wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki nchini humo,hivyo amekiri kuwa mmoja wa waathiriwa wa uchawi.
Hata hivyo wadau wa muziki wanahoji kwamba matatizo ya ziza bafana yametokana na uraibu wa madawa ya kulevya, hivyo amekuwa akiishi maisha ya uchochole tangu hatengane na aliyekuwa meneja wake Roger Lubega.