Staa wa muziki wa Bongofleva Ali Kiba ametangaza kuirudisha akaunti yake ya YouTube iitwayo “AliKiba” ambayo alikuwa ameacha kuitumia kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi 10.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, King Kiba ameandika kwamba akaunti hiyo imerudi na kuwaomha mashabiki zake Wa-Subscribe kwani kuna mengi yanakuja kwa mwaka huu ikiwemo album yake mpya.
Video ya mwisho kupandishwa kwenye chaneli hiyo yenye zaidi ya views 124M, ilikuwa ni MBIO ambayo aliiweka tarehe 26 mwezi April mwaka wa 2019.
Kuna taarifa za chini ya kapeti zinasema kwamba sababu zilizopelekea Ali Kiba kuiacha chaneli hiyo ni kubanwa na vipengele vya mikataba aliyokuwa amesaini na Seven Mosha ambaye alikuwa meneja wake.
Hivyo kwa kipindi chote hicho alikuwa akitumia chaneli ya King’s Music Records kuweka video zake.