SERIKALI YAWEKA MIKAKATI DHABITI YA KUKABILIANA NA KUPANDA KWA VISA VYA MIMBA ZA MAPEMA KAUNTI YA TRANS NZOIA

You are currently viewing SERIKALI YAWEKA MIKAKATI DHABITI YA KUKABILIANA NA KUPANDA KWA VISA VYA MIMBA ZA MAPEMA KAUNTI YA TRANS NZOIA

Serikali imewanasa na kuwafungulia mashtaka watu 307 katika oparesheni ya kukabiliana na wanaohusika katika visa ya mimba za mapema katika Kaunti ya Trans nzoia. 

Kamishna wa Kaunti hiyo Sam Ojwang amewaagiza machifu na manaibu wao kuendeleza oparesheni hiyo vijijini haswa wakati huu ambapo Wanafunzi wamefunga shule katika likizo ndefu ya wiki saba. 

Wazazi pia wameonywa dhidi ya kuwakinga wanaoendeleza visa vya mimba za mapema, kwani wao pia watashtakiwa kwa makosa ya kutoripoti uhalifu na kujipata pabaya.

Wakti huwo huo Ojwang anasema kamati maalum itabuniwa kuangazia visa vya mimba za mapema na kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka. 

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.