MATUMAINI YA WAZANZIBARI KATIKA URAIS WA SAMIA SULUHU HASSAN

You are currently viewing MATUMAINI YA WAZANZIBARI KATIKA URAIS WA SAMIA SULUHU HASSAN

Licha ya huzuni iliyotanda Tanzania na Zanzibar, kufuatia kifo cha Rais John Magufuli, Wazanzibari wamepata matumaini makubwa baada ya kuapishwa kwa Mzanzibari mwenzao Samia Suluhu Hassan kuwa rais wa muungano.

Baada ya kuapishwa kwa Mama Samia, watu mbali mbali walifuatilia matangazo ya moja kwa moja yaliokuwa yakirushwa na vituo vya televisheni na kuonesha kufurahishwa kwao.

Baadhi ya watu walikuwa wakitoa kauli za kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo iliyofikiwa huku wengi wakitoa maoni yao kuonesha matumaini makubwa na kumtakia kheri kwenye utumishi wake.

Watu ambao amefanya nao kazi wanamzungumzia Rais Samia kuwa ni mchapakazi, msikivu, mwenye tabia ya kuheshimu maamuzi yanayotokana na vikao na mtoaji maamuzi yasioumiza kutokana na kutumia busara zaidi kwenye uamuzi wake.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.