Ili kuwahamasisha Wananchi kuhusu ubora wa chanjo dhidi ya COVID-19, Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari na Makamu wake Yemi Osibanjo wamekuwa watu wa kwanza kupatiwa chanjo.
Baada ya kupatiwa chanjo, Rais Buhari alitumia fursa kuwaomba Wananchi wa Nigeria kufahamu umuhimu wa kupatiwa chanjo ili kujikinga na Corona Virus kama yeye alivyofaya pamoja na Makamu wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais juu ya COVID-19, Boss Mustapha amesema uongozi wa Nigeria una imani kwa chanjo zilizoagizwa kutoka nje na kwamba hazina madhara.
Nigeria ilipokea chanjo ya COVID19 huku kampeni ikiendelea kuelimisha Wananchi kuhusu COVID-19 na hatua za msingi za kuchukuliwa kuzuia na maambukizi