Shirika la afya duniani (WHO) linasema kwamba janga la virusi vya corona halina uwezekano wa kumalizika katika miezi ya karibuni.
Mkurugenzi wa Mpango wa dharura wa shughuli za kiafya WHO, Michael Ryan, amesema anadhani ni mapema kufikiria kwamba watalimaliza janga hili kufikia mwishoni mwa mwaka.
Aidha amesema kinachoweza kumaliza janga hilo ni ikiwa ulimwengu utakuwa makini na idadi ya watu wanaolazwa hospitalini kutokana na virusi hivyo au vifo na matatizo mengine yanayosababshwa na janga hilo.
WHO imetoa wito kwa Nchi mbalimbali kujiepusha kuondoa haraka shughuli za kudhibiti virusi vya corona, kutokana na kuwepo chanjo.