Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca ambapo chanjo ilitakiwa kuanza Machi 15.
DRC imeshapokea dozi milioni 1.7 za chanjo lakini Serikali imesema imesitisha kama tahadhari baada ya Nchi kadhaa kusitisha utoaji wa chanjo hiyo.
Serikali imesema tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hiyo itatangazwa baada ya uchunguzi wa Kiserikali na wa Kimataifa.
Denmark, Norway, Bulgaria, Thailand na Iceland zimesema chanjo hiyo inasababisha Kuganda kwa Damu huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisisitiza kuwa chanjo hiyo ni Salama