Vyombo vya Usalama nchini Urusi vimewakamata Wanasiasa 200 wa Upinzani na Viongozi wa Manispaa waliokuwa kwenye mkutano Mjini Moscow.
Mkutano huo uliowakutanisha Viongozi na Wafuasi wa Upinzani kutoka majimbo 50 ya Urusi ulivamiwa na Polisi na kuwakamata washiriki ikiwemo Viongozi Waandamizi wa Upinzani pamoja na Waandishi Habari.
Walikusanyika kujadili Uchaguzi wa Bunge na Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Septemba 2021. Aidha, zaidi ya Waandamanaji 1,000 nao wako mikononi mwa Polisi