MSIJIHUSISHE NA UTOVU WA NIDHAMU, WATAHINIWA WA KCPE NA KCSE WAONYWA

You are currently viewing MSIJIHUSISHE NA UTOVU WA NIDHAMU, WATAHINIWA WA KCPE NA KCSE WAONYWA

Watahiniwa wa mitihani ya Kitaifa katika Kaunti ya Pokot Magharibi wametakiwa kudumisha nidhamu msimu huu ili kuchochea matokeo mema.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya kipekee katibu wa KNUT tawi la Pokot Magharibi Martin Henrico Sembelo amekashifu visa vya wanafunzi kujihusisha katika matumizi ya dawa za kulevya akiwataka kuweka mawazo yao katika mitihani na kutia bidii.

Aidha Sembelo ametoa wito kwa wazazi kuwapa wanao ushauri nasaha msimu huu wa likizo akisema ndo njia ya pekee ya kuepuka visa vya mimba na ndoa za mapema miongoni mwa wasichana wenye umri mdogo.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.