VILIO VYATAWALA WAKATI WA KUAGWA MWILI WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

You are currently viewing VILIO VYATAWALA WAKATI WA KUAGWA MWILI WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaongoza viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, mawaziri na wananchi kumuaga aliyekuwa Rais wa Taifa hilo John Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu, jijini Dar es salaam kutokana na tatizo la mfumo wa umeme kwenye moyo.

Rais Suluhu ambae ameapishwa kushika wadhifa huo siku ya ijumaa baada ya kifo cha mtangulizi wake dokta John Magufuli, macho yake yalionekana kudhoofika na kuchoka aliketi mita chache kutoka lilipokuwa jeneza la hayati Magufuli na mjane wake Janeth Magufuli.

Vilio na majonzi vilitawala katika uwanja wa Uhuru, ambapo shughuli ya kutoa heshima ya mwisho kwa kiongozi huyo alieonekana kuwa na misismamo ya kujitegemea kiuchumi zilifanyika.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.