WAKULIMA WAPOKEA MBEGU YA MAHINDI KUTOKA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

You are currently viewing WAKULIMA WAPOKEA MBEGU YA MAHINDI KUTOKA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Gavana Lonyangapuo[kulia] akimkabidhi mwenyeji mbegu ya mahindi

Katika juhudi za kukabiliana na uhaba wa chakula katika Kaunti ya Pokot Magharibi, Serikali ya Kaunti hiyo inaendeleza mikakati ya kuwapa wakulima mbegu.

Gavana John Lonyangapuo anasema amechukua hatua hiyo ili kupunguza visa vya wananchi kutegemea misaada ya chakula kutoka kwa wahisani kwani wananchi wanaweza kuzalisha vyakula vya kutosha.

Lonyangapuo anasema Serikali yake itaendelea kuwekeza kwa wananchi ili kuzima kabisa visa vya wizi wa mifugo na kuhakikisha wananchi wanajiimarisha kupitia kilimo na ufugaji.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.