Nchi ya Canada ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola ya Mataifa ya Uingereza, takriban nusu ya watu wameitaka Nchi yao iwakilishwe na Rais atakayechaguliwa badala ya Malkia wa Uingereza
Asilimia 45 ya Wananchi wa Canada walioshiriki mchakato ulioandaliwa na wakala wa utafiti wa kura ya maoni, wamesema wanapendelea kuwa na Rais wa Nchi aliyechaguliwa kupitia Uchaguzi
Wakati asilimia 24 ya wahojiwa walionekana kupendelea Canada ibaki ya kifalme, asilimia 18 walisema hawajali hata kidogo juu ya suala hili na asilimia 13 walikosa maamuzi.