NIGERIA: RAIS AWAPA RUHUSA WANAJESHI YA KUWAPIGA RISASI WAMILIKI WA BUNDUKI AK-47

You are currently viewing NIGERIA: RAIS AWAPA RUHUSA WANAJESHI YA KUWAPIGA RISASI WAMILIKI WA BUNDUKI AK-47

Rais Muhammadu Buhari ametoa agizo kwa Wanajeshi wa Nigeria kwa kuwapa ruhusa ya kuwapiga risasi bila kuhitaji kibali, Watu wote watakaoonekana wakiwa na bunduki aina ya AK-47.

Amri hii imetolewa kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama, baada ya matukio matatu ya utekaji nyara kati ya Desemba 2020 na Februari 2021 ambapo magenge ya wahalifu yaliwachukua mateka mamia ya Wanafunzi.

Desemba mwaka wa 2020 wavulana zaidi ya 300 walitekwa katika Shule ya Bweni Mjini Kankara, na Februari mwaka wa 2021 idadi kama hiyo ya wasichana walichukuliwa mateka kutoka Shule ya Jangebe.

Wasichana hao wengi wameshapatikana, lakini Wavulana wote hawajulikani walipo. Watekaji katika matukio hayo huja wakijihami kwa bunduki chapa AK-47.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa