MYANMAR: KIONGOZI WA CHAMA CHA NLD AFARIKI AKIWA MIKONONI MWA POLISI

You are currently viewing MYANMAR: KIONGOZI WA CHAMA CHA NLD AFARIKI AKIWA MIKONONI MWA POLISI

Zaw Myat Linn ni kiongozi wa pili wa Chama cha National League for Democracy (NLD) kufariki akiwa mikononi mwa polisi. Wanasisa wanadai kuwa alipigwa sana baada ya kukamatwa siku ya Jumanne.

Mamalaka zimesema Zaw Myat Linn alifariki Yangon ambapo alikuwa ni mstari wa mbele sana katika kuongoza maandamano ya kupinga Mapinduzi ya Kijeshi.Kiongozi mwingine aliyefariki baada ya kukamatwa ni Khin Maung Latt.

Aidha, watu zaidi ya 60 wamefariki kutokana na maandamano yanayoendelea huku wengine takriban 2000 wakiwa wamekatwa.

Jeshi Nchini Myanmar lilimkata Rais Aung San Suu Kyi, Februari 1 na kuanza kuongoza nchi hiyo kijeshi na kuendelea kushikilia Mamlaka japo Wananchi wanaandamana kutaka Utawala wa Demokrasia

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa