BOB WINE MASHAKANI KWA KUWA NA GARI LA KIFAHARI AMBALO HALIINGI RISASI.

You are currently viewing BOB WINE MASHAKANI KWA KUWA NA GARI LA KIFAHARI AMBALO HALIINGI RISASI.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine amejipata mashakani kwa madai ya kuwa na gari ambalo haliingii risasi.

Hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo ambapo Gari hilo limevutia mamlaka nchini Uganda, huku mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru ya Uganda (URA) ikisema maelezo yaliyotolewa si sahihi na kwamba thamani yake iko chini kuliko inavyostahili kuwa.

URA, sasa inataka gari hilo kukaguliwa upya. Bobi Wine, hata hivyo amekataa kuwasilisha gari hilo kwa misingi kwamba agizo hilo haliambatani na sheria, kulingana na taarifa yake iliyonukuliwa na gazeti la Daily Monitor.

Gari hilo liliingizwa nchini na kusajiliwa Kenya mwaka jana na kisha kupelekwa Uganda kupitia mpaka wa Busia.

Katika ujumbe alioweka mtandaoni Februari 21, Bw. Kyagulanyi alidai kuwa gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilitolewa kwake kama msaada na marafiki na wafuasi wake nchini Unganda na ughaibuni:

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa