Asilimia 51.2 ya Wananchi nchini Uswisi wamepiga kura ya maoni kuunga mkono marufuku ya kuvaa Hijabu katika maeneo ya Umma ikiwemo ‘Burka’ na ‘Niqab’ zinazovaliwa na Wanawake wa Kiislamu
Asilimia 48.8 wamepingwa Muswada huo uliowasilishwa na Mrengo wa Kulia wa Chama cha Swiss People’s Party ambacho kilifanya kampeni yake kwa kutumia misemo kama vile “Sitisha itikadi kali”
Baraza la Waislamu Nchini Uswisi limesema Uamuzi huo umefungua vidonda vya kale, na kuongeza pengo la ukosefu wa usawa kisheria na ishara ya wazi ya kutengwa kwa Kundi la Waislamu walio wachache.
Serikali imejitetea dhidi ya marufuku hiyo kwamba siyo jukumu la Serikali kuamua kile watakachovaa Wanawake.