Vyombo vya Usalama Uganda vimetakiwa kutoa taarifa za watu waliokamatwa wakati wa Kampeni 2020 ili wafahamike na Familia zao ziweze kujua walipo na kuwafikia.
Rais Museveni amesema kipindi cha Uchaguzi kulikuwa na kundi la wahalifu waliopanga kuvuruga Amani, akalazimika kuongeza Usalama na kuweka kikosi cha makomandoo waliokamata Vijana 59, na Vikosi vya Usalama vikawakamata wengine 65.
Vilevile, Kiongozi huyo amezilaumu Jamii za Kimataifa kwa kuingilia masuala ya ndani ya Taifa la Uganda