WAZIRI MKUU WA CONGO AJIUZULU

You are currently viewing WAZIRI MKUU WA CONGO AJIUZULU

Waziri mkuu wa Congo Sylvestre Ilunga Ilunkamba amewasilisha barua kwa Rais Felix Tshisekedi kutaka kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu.

Ilunga ameongoza Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano kwa miezi 15. Wabunge walipiga Kura ya kutokuwa na Imani na Serikali yake Januari 27, na walimpa saa 24 kujiuzulu.

Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Rais Tshisekedi kuwateua washirika wake kama Mawaziri. Awali, alikuwa akidhibitiwa na Muungano alionao na Rais Kabila ambao uliafikiwa alipoingia madarakani.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa