Waziri wa Afya Nchini humo, Dkt. Jane Ruth Aceng amesema Rais Yoweri Museveni na watu wake wa karibu hawajapatiwa chanjo dhidi ya Virusi vya Corona.
Wizara ya Afya imetoa kauli hiyo ikikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Uganda la Daily Monitor na The Wall Street Journey la Marekani zikidai Museveni na watu wa karibu naye wamepata Chanjo.
Hadi sasa Nchi hiyo imerekodi maambukizi 40,243 na vifo 333 huku waliopona wakifikia 14,615