Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki Dunia hii leo akiwa Hospitali ya Muhimbili Nchini Tanzania alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kabla ya kifo chake alitangazwa na Chama cha ACT-Wazalendo kuwa alipata maambukizi ya COVID 19 na alikuwa akiendelea vizuri na matibabu.
Mwanasiasa huyo alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo. Pia, amewahi kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF)
Kutokana na kifo hicho, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza siku 7 za maombolezo.