RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA, AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3

You are currently viewing RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA, AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3
Former French President Nicolas Sarkozy, wearing a protective face mask, arrives for the verdict in his trial on charges of corruption and influence peddling, at Paris courthouse, France, March 1, 2021. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi.

Hukumu hiyo iliyotolewa jana na mahakama mjini Paris inajumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje.

Sakorzy alikuwa anashtakiwa kwa kujaribu kupata taarifa za ndani kinyume cha sheria kuhusu uchunguzi juu ya ufadhili wa kampeni zake kutoka kwa jaji mwaka 2014.

Mahakama hiyo imesema Sarkozy atakuwa na haki ya kuomba kuzuiliwa nyumbani kwa kutumia bangili ya umeme.

Washtakiwa wenzake wawili ambao ni wakili Thiery Herzog na jaji Gilbert Azibert, pia wamekutwa na hatia na wamehukumiwa kifungo sawa na chake.

Baadae mwezi huu, Sarkozy atakabiliwa na kesi nyingine pamoja na watu wengine 13 kwa mashtaka ya kufadhili kinyume cha sheria kampeni yake ya urais mwaka 2012.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa