Baraza la Seneti limepiga kura kuidhinisha mpango wa Dola za Marekani Trilioni 1.9 unaolenga kuwasaidia Wamarekani kukabiliana na athari za mlipuko wa COVID-19.
Mpango huo umepitishwa kwa kura 50-49 na utarudishwa kwa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kupitishwa kuwa Sheria na baada ya hapo utasainiwa na Rais Joe Biden.
Marekani ni Taifa lililoathiriwa zaidi na janga la Virusi vya Corona ambapo watu wapatao 523,000 wamepoteza maisha huku Milioni 29 wakipata maambukizi.