Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi amewasilisha rufaa iliyorekebishwa mahakamani kama hatua ya kuzidisha uzito wa ushahidi wake kupinga kisheria ushindi wa Rais Yoweri Museveni.
Sambamba na hilo upande wa Rais Museveni umepinga hatua ya kurekebisha shauri hilo ambalo mahakama ya juu inatakiwa kushungulikia na kutoa maamuzi yake kabla ya mwezi Mei ambapo rais mteule anatakiwa kuapishwa.
Tume ya Uchaguzi ya Uganda pamoja na mawakili wa Rais Museveni wamepinga kurekebishwa kwa rufaa hiyo. Wametoa angalizo kuwa hatua ya upande wa Kyagulanyi kutaka kuongezea ushahidi ili kuonyesha kuwa sheria fulani za uchaguzi zilikiukwa ni suala ambalo hawakubaliani nalo.