Ikulu ya Marekani imeonesha wasiwasi wake baada ya shambulio dhidi ya huduma ya Exchange ya Microsoft na kuzitaka Taasisi Binafsi na za Serikali zilizoathiriwa kuchukua hatua za haraka ili kuepusha madhara zaidi.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki ametaja kitendo cha udukuzi kwenye ‘server’ za Microsoft kuwa shambulio la wazi, akisema mianya iliyoonekana katika ‘server’ hizo zilizotumiwa na wadukuzi inaweza kuwa na madhara zaidi.
Microsoft imeilaumu China kufadhili shambulio hilo la kidigitali ambalo limeathiri maelfu ya Taasisi Nchini Marekani.