Mwanamuziki wa bendi nchini Uganda Sophia Gombya amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu utofauti kati yake na msanii ykee benda.
Akipiga stori na runinga ya NBS Gombya amesema Ykee Benda ni mtu wa wivu ambaye uhisi vibaya pindi wasanii wengine nchini Uganda wakimtambua kama rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo.
Aidha amesisitiza kuwa hana ugomvi wowote na mkali huyo wa ngoma ya “Eva” huku akisema kwamba huwa anaumia sana wanamuziki wengine wakimvunjia Ykee Benda heshima lakini pia amekiri kuwa sio makosa yake watu wanapomuita rais wa muungano huo.
Ikumbukwe Sophia Gombya alijuzulu mwishoni mwa mwaka wa 2020 kama rais wa muuungano wa wanamuziki nchini Uganda wadhfa ambao Ykee Benda aliuchukua lakini baada ya miezi kadhaa alijiondoa kwa madai kwamba wasanii wengi nchini humo wanamdharau.