Wakati ukichukulia poa siku ya Valentines, huko nchini Marekani rapa Offset hakuwa na jambo dogo kwa Baby Mama wake Cardi B , kwani amempatia zawadi ya mkoba wenye thamani ya shillingi millioni 2.2.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cardi B ametoa shukrani za dhati kwa mumewe kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea, sambamba na kuonyesha mkoba huo pamoja na bei kupitia risiti ya manunuzi.
“Wow Asante mpenzi (Offset). Mara nyingi unaniletea vitu vya kitofauti nakupenda na nakuheshimu sana”. Aliandika #CardiB kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hii sio mara ya kwanza kwa Offset kumnunulia mkewe zawadi za mkwanja mrefu kwani miezi minne iliyopita alimzawadia gari la zaidi ya shillingi millioni 47.