Ikiwa tayari ni miaka minne imepita tangu nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido aachie hit song yake iitwayo “IF”, good news ni kwamba hadi kufikia sasa ngoma hiyo tayari imeshagonga Gold kwenye mauzo yake sokoni, yaani imeuza nakala zaidi ya laki tano kwa Marekani.
Kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimetoa taarifa hiyo kupitia tovuti yake huku ikisubiriwa Davido kukabidhiwa cheti chake.
“IF” umeweka rekodi ya kuwa wimbo wa pili wa mahadhi ya Afro beat ulioimbwa na msanii mmoja (Solo song) kufikisha kiwango hicho cha mauzo kwa Marekani.
Haya hivyo, “IF” unakua wimbo wa pili kwa Davido baada ya “FALL” ambao nao ulifikia kiwango cha mauzo ya Gold, Mei 28, 2020.