RAGGA DEE ADAI CHUKI MIONGONI MWA WASANII NDIO KIKWAZO KWA MUZIKI WA UGANDA KUFIKA KIMATAIFA.

You are currently viewing RAGGA DEE ADAI CHUKI MIONGONI MWA WASANII NDIO KIKWAZO KWA MUZIKI WA UGANDA KUFIKA KIMATAIFA.
  • Post category:Burudani

Msanii nguli wa muziki nchini uganda Ragga Dee amedai kwamba wasanii wengi nchini humo wanachukiana na ndio maana wengi wao muziki umewashinda.

Akiwa kwenye moja ya Interview Ragga Dee  amesema kuwa wasanii wa  uganda wanatumia muda wao mwingi kuharibiana majina badala ya kutoa muziki mzuri ambao utatoa elimu kwa jamii.

Hata hivyo ametoa wito kwa wasanii kuacha kadhia ya kuwazusha wasanii wenzao na badala yake waelekeze nguvu zao kwenye suala la kujenga tasnia ya muziki nchini humo ili iweze kufikia viwango vya kimataifa.

Ikumbukwe Ragga Dee ni mmoja wa wasaani wakongwe kwenye kiwanda cha muziki nchini uganda na licha ya kutotoa muziki kila mara msaani huyo anatajwa kuwa mmoja wa watu tajiri nchini uganda.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa