Msanii wa muziki nchini Otile Brown ameamua kuwashauri wasanii wenzake ambao kwa namna moja ama nyingine baada ya kupata umaarufu walio nao wamejisahau na kuwasahau baadhi ya watu waliokuwa karibu nao kipindi hawajaupata umaarufu huo.
Kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Otile Brown amewataka wasanii kuacha tabia ya kuwadharau watu kwa sababu ya umaarufu walio nao kwani ni watu hao ndio wanawapa support ambayo imechangia ukuwaaji wao kisanaa.
Haijebainika ni kitu gani kilimsukuma hitmaker huyo wa ngoma ya “Regina” kuzungumzia suala hilo ila wajuzi mambo wanahisi kwamba huenda msanii huyo anatafuta huruma kutoka kwa mashabiki au ana kazi mpya ambayo inazungumzia ishu ya usanii na umaarufu.