MEMBER WA KUNDI LA ELANI “MAUREEN KUNGA” AFUNGUKA ALIVYOKUWA ANACHUKIA TABASAMU LAKE.

You are currently viewing MEMBER WA KUNDI LA ELANI “MAUREEN KUNGA” AFUNGUKA ALIVYOKUWA ANACHUKIA TABASAMU LAKE.
  • Post category:Burudani

Member wa kundi la Elani maureen Kunga amefunguka namna ambavyo mapungufu yake kimwili yalimpelekea kuchukia sana tabasamu lake ambalo lilimfanya kuwa na aibu kila mara akiwa mbele ya watu.

Kupitia post ndefu aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo amesema kipindi hicho alikuwa anahisi meno yake ni ndogo sana, hivyo haviendani na vigezo vya urembo ambavyo ulimwengu sasa umekumbatia.

Aidha amedokeza kwamba alikuja akajikubali baada ya kutiwa moyo na marafiki pamoja na wanafamilia wake wa karibu, hivyo aibu aliyokuwa nayo juu ya tabasamu lake lilitoweka.

Hata hivyo baada ya kuweka hilo wazi,mashabiki zake  pamoja na watu maarufu nchini walionekana kuguzwa na changamoto aliyokumbana nayo katika maisha huku wakisema kuwa ujumbe huo utawapa moyo wanaojiona kwamba hawafai katika jamii kutokana na mapungufu ya muonekano wao wa kimwili.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa