WILSON LONYANGOLE: MVUA KUCHELEWA KUFUATIA KIMBUNGA KENNETH.

You are currently viewing WILSON LONYANGOLE: MVUA KUCHELEWA KUFUATIA KIMBUNGA KENNETH.

Wakulima kazikazini mwa Bonde la Ufa na magharibi ya nchi wamehimizwa kutopanda mimea yao mapema kwa kuchelewa kwa mvua za masika kutokana na kimbunga ambacho kimetabiriwa kukumba mpaka wa taifa la Msumbiji na Tanzania.

Kulingana na ripoti ya Mkurungenzi mkuu wa idaya ya utabiri ya wa hali ya hewa gatuzi la Pokot Magharibi Wilson Lonyangole, ujio wa kimbunga hicho kumechelewesha kuanza kunyesha kwa mvua ambayo ilitabiriwa kuanza wiki ya pili ya mwezi huu wa tatu na wakulima sasa wanafaa kusubiri kuhusu ni lini wakati mwafaka wa kurejea shambani kwa msimu wa upanzi mwaka 2021, wataalamu wa hali ya hewa wamezungumzia hali hiyo.

Kwa mjibu wa Lonyangole, huenda mvua itachelewa kwa siku kumi zaidi nani vema wakulima kuendelea kuandaa mashamba kusubiri ripoti ya idara hiyo nao maafisa wa nyanjani wakitakiwa kuwashauri wakulima vilivyo kuhusu mbegu na mbolea.

Aprili mwaka 2019 Msumbiji ilikabiliwa na mvua kubwa na upepo mkali baada ya kimbunga Kenneth kukumba taifa hilo na kusababisha mvua kuchelewa kwa muda mrefu katika mataifa kadhaa ya afrika mashariki na kati.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa