Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi kwa ushirikiano na shirika la Kenya smart climate limetoa kondoo zaidi ya mia moja kwa wakaazi wa Siyoi.
Waziri wa kilimo kaunti hiyo Godfrey Lipale anasema kondoo hao wamefanyiwa utafiti na wana uwezo wa kuzaana mara mbili kwa mwaka kando na kuwapa wananchi maziwa yenye madini akisema wakulima watafaidi pakubwa.
Aidha anasema wakulima ambao wamekaguliwa na kuidhinishwa na Wizara ya kilimo ndio watakaofaidi na kondoo hao.