VIONGOZI KAUNTI YA BARINGO WATAKA SERIKALI KUWEKEZA ZAIDI KATIKA SEKTA YA ELIMU

You are currently viewing VIONGOZI KAUNTI YA BARINGO WATAKA SERIKALI KUWEKEZA ZAIDI KATIKA SEKTA YA ELIMU

Serikali ya kitaifa imetakiwa kushirikiana na ile ya Kaunti ya Baringo kuwekeza katika maswala ya elimu kama njia moja ya kumaliza visa vya uhalifu katika eneo la Tiaty.

Mwakilishi wa wadi ya Tirioko Sam Lokales anasema asilimia kubwa ya vijana katika eneo hilo hawajakumbatia elimu hivyo pana haja ya Wenyeji kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa elimu akisema itasaidia pakubwa kupunguza visa vya uhalifu na kurejesha taswira nzuri kuhusu Jamii ya Pokot.

Amekariri msimamo wa viongozi katika kuanti hiyo kufanikisha mchakato wa kupatikana kwa amani ya kudumu na kuhakikisha wananchi wanakumbatia maendeleo.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.