Wizara ya Afya kaunti ya Turkana imeanzisha huduma tamba kwenye eneo la Caanan lililoko kwenye wadi ya Kanamkemer ili kuwatibu wakazi wa eneo hilo ambao walikuwa wanatembea kilomita mingi kutafuta matibabu katika hospitali ya rufaa ya Lodwar.
Afisa mkuu mpya katika wizara hiyo Augustine Lokwang amedokeza kuwa afisi yake inapania kuwapiga jeki wahudumu wa afya wa vijijini kando na kuboresha miundo msingi na mbinu katika sekta ya afya.
Hospitali ya Caanan ilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali kuwa ni kituo cha karantini kwa wagonjwa wa covid 19.