Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuna hatari kubwa ya mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola uliopo Guinea kusambaa Mataifa jirani. Shirika hilo limesema baadhi ya Nchi hizo hazijajiandaa kwa kampeni za Chanjo.
Mwakilishi wa WHO Guinea, Gerorges Alfred Ki-Zerbo amesema visa 18 vimerekodiwa hadi sasa na kati yao, wanne wamepoteza maisha. Tayari watu 1,604 wamepatiwa chanjo dhidi ya Ugonjwa huo ambao umeibuka tena hivi karibuni.