UTAFITI: WANAUME WANAATHIRIWA ZAIDI NA COVID-19 KULIKO WANAWAKE.

You are currently viewing UTAFITI: WANAUME WANAATHIRIWA ZAIDI NA COVID-19 KULIKO WANAWAKE.

Umoja wa Mataifa umesema Virusi vya Corona vinasababisha vifo kwa Wanaume wengi zaidi Barani Afrika kuliko Wanawake ambao wao wanaandamwa na kupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi.

Utafiti uliofanyika kwenye Nchi 28 za Afrika, ikiwemo Guinea, Mauritius na Uganda umeonesha kwa wastani idadi ya Wanawake waliopata maambukizi au kufa kwa corona ni ndogo ikilinganishwa na Wanaume.

Takwimu zinaonesha asilimia 41 ya Wanawake Barani Afrika ndiyo wamekumbwa na Janga la Corona lakini idadi hiyo inatofautiana miongoni mwa Mataifa.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema kwa Wanawake janga la COVID-19 limesababisha ukosefu wa huduma za uzazi.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa