CHAMA CHA BOB WINE CHASHINDA VITI VINGI VYA UMEYA KULIKO CHA MUSEVENI.

You are currently viewing CHAMA CHA BOB WINE CHASHINDA VITI VINGI VYA UMEYA KULIKO CHA MUSEVENI.

Chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’, kimekishinda mbali Chama cha Rais Yoweri Museveni cha National Resistance Movement (NRM) katika chaguzi za Kampala Capital City Authority (KCCA).

Kwa mujibu wa Gazeti la The Independent nchini Uganda, NUP kilishinda viti 41 kati ya 44 vya umeya na hivyo kukiacha mbali chama tawala.

Viti vitatu vilivyosalia vilichukuliwa na chama kinachohusiana na mgombea wa zamani wa Urais, Kizza Besigye cha Forum for Democratic Change (FDC).

Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa chama kinachoongozwa na Rais Museveni, NRM na Democratic Party (DP) kushindwa katika uchaguzi wa Umeya Kampala.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa