Ripoti ya Intelijensia ya Marekani imesema Mwanamfalme wa Saudi, Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya Mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi yaliyotokea mwaka 2018.
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo iliyotolewa chini ya Utawala wa Rais Joe Biden, imeelezwa Mwanamfalme alipitisha mpango wa kumkamata au kumuua Mwanahabari huyo. Khashoggi aliuawa ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia Mjini Istanbul, Uturuki.
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya watu mbalimbali Saudi Arabia isipokuwa Mwanamfalme Salman. Saudi Arabia imepinga Ripoti hiyo ikisema ni ya uongo na haikubaliki.