Watawala wa Jeshi Nchini Myanmar wamemfuta kazi Balozi wa Taifa hilo wa Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa ni siku moja baada ya kauli yake ya kuomba msaada ili Jeshi liondolewe madarakani.
Katika hotuba yake, Kyaw Moe Tun alisema watu wote wasishirikiana na Jeshi mpaka madaraka yatakaporejeshwa kwa Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.
Vilevile, Balozi huyo alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kutumia mbinu zozote kuchukua hatua dhidi ya Jeshi ili kusaidia kurejesha Demokrasia, akisema anawakilisha Serikali ya Aung San Suu Kyi iliyotolewa madarakani.