Watu 500 wamejeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea karibu na Kambi za Wanajeshi, Mji Mkuu wa Bata, Machi 8 huku watu wengine 15 wakiripotiwa kufariki.
Rais Teodoro Obiang Nguema amesema milipuko hiyo imesababishwa na uzembe uliohusishwa na hifadhi ya baruti kali kambini.
Amesema athari iliyotokana na milipuko ni pamoja na uharibifu mkubwa katika nyumba zote na majengo yaliyo karibu na Kambi ya Jeshi na hivyo ameomba usaidizi wa kimataifa.
Aliongeza kwamba, huenda tukio hilo limetokea kufuatia hatua ya wakulima kuchoma mashamba yanayozunguka Kambi za Jeshi