Ripoti ya 2021 ya Inter Parliamentary Union imeonesha Tanzania inaongoza kwa kuwa na Wabunge Wanawake wengi ukilinganisha na Kenya na Uganda. Tanzania ina Wanawake 36.7% ya Bunge hivyo iko nafasi ya 34 kidunia.
Uganda imeonekana kuwa na Wabunge Wanawake 34.9% na iko nafasi ya 37 kidunia huku Kenya ikiwa na Wabunge Wanawake 21.6% na kuwa nafasi ya 107.
Rwanda na Burundi wako nafasi nzuri zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki, kwani Rwanda ina Wanawake 61.3% Bungeni ambapo ni ya kwanza kwa kuwa na Wabunge Wanawake wengi duniani.
Burundi ina Wanawake 38.2% Bungeni ambapo iko nafasi moja juu ya Tanzania