Waziri wa fedha katika kaunti ya Uasin Gishu Julius Ruto ameitetea kaunti hiyo dhidi ya madai kwamba ilifeli kutumia shilingi bilioni tatu nukta mbili zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa kifedha 2018/2019.
Kulingana na Ruto japo pesa hizo zilikuwa zimetengwa na kujumishwa kwenye bajeti ya mwaka ziliwasilishwa baada ya mwaka wa kifedha kukamilika na hivyo hazikutumika kama ilivyokusudiwa.
Aidha amesema kuna baadhi ya miradi ambazo zinachukua muda kukamilika na hivyo fedha zilizotengwa kuifanikisha hazikutumika