Wafugaji wa ngombe wa maziwa katika kaunti ya Vihiga wamepigwa jeki baada ya kaunti hiyo kutoa ng’ombe 47 kwa makundi ya wakulima mbalimbali ili kuimarisha uzalishaji wa kiwango cha maziwa.
Gavana wa kaunti hiyo Wilber Otichilo ametoa changamoto kwa wakulima kujisatiti ili kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka.
Katika kipindi cha miaka mitatu kaunti hiyo imepeana zaidi ya ngombe 250 wa maziwa bila malipo kwa makundi ya wakulima.
Hata hivyo wakulima wanasema kwamba hatua hiyo itawasaidia pakubwa kuwapa ajira.
Kadhalika gavana Otichilo amewashauri wakulima kuwasiliana na kitengo cha kilimo kaunti hiyo iwapo watahitaji ushauri kuhusu kilimo.
Kulingana na gavana Otichilo, anapanga kujenga kiwanda cha maziwa ili kuinua kipato cha wakulima wanaopatikana eneo hilo,