Mamlaka ya Kilimo na Chakula nchini imedai uchunguzi umebaini kuwa mahindi yanayoingia kutoka Tanzania na Uganda sio salama kwa matumizi ya binadamu.
Imedai kuwa, mahindi hayo yana kiwango kikubwa cha sumu hasa aflatoxins na fumonisins ambazo zinajulikana kusababisha Saratani.
Mamlaka hiyo imedai, Sumu hizo zimesababisha vifo vya Wakenya wengi kwa miaka, hali iliyosababisha wachukue hatua ya kuacha kupokea mahindi kutoka Tanzania na Uganda.
Aidha, imesema wataendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na nchi wanazoshirikiana nazo kibiashara na wanasubiri kuona washikadau wakilizungumzia tatizo hilo