KENYA YATAJWA KUWA KITOVU CHA UTAKATISHAJI FEDHA AFRIKA MASHARIKI

You are currently viewing KENYA YATAJWA KUWA KITOVU CHA UTAKATISHAJI FEDHA AFRIKA MASHARIKI
  • Post category:Biashara

Ripoti ya Bureau of International Narcotics and Law Enforcement Affairs imeitaja Kenya kuwa Kitovu cha Utakatishaji Fedha ambao hufanyika kwa Taasisi rasmi na zisizo rasmi.

Kenya imetajwa kuwa na wafadhili wa ugaidi, vikundi vya uhalifu wa kimataifa, uhalifu wa mtandaoni, uharamia na biashara haramu ya mali pori.

Ripoti imetaja ukaribu wa Kenya na Somalia kijiografia kunaifanya nchi hiyo itumike zaidi kwa Biashara Haramu na kuwa njia kuu ya Dawa, Kuuza Watu na Wanyama Pori.

Aidha, ripoti hiyo imeisifia Tanzania kwa kuwa na sheria ya kuthibiti utakatishaji fedha huku ikitajwa kuwa na changamoto ya kitaasisi kudhibiti ukwepaji kodi na rushwa

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa