Prodyuza wa muziki nchini Uganda Washington amefunguka na kusema kwamba kifo cha msanii Mozey Radio imeathiri pakubwa kazi yake kutayarisha muziki.
Akiwa kwenye moja interview Washington amesema kwa sasa hafanyi suala la kutayarisha muziki kwa moyo wake wote kama miaka hapo nyuma kwani alipoteza hamu ya kutayarisha muziki baada ya kifo cha Mozey Radio.
Ikumbukwe Washington ni moja kati ya maprodyuza waliondaa ngoma kali za Mozey Radio kama “Dont Cry” na “Breathe Away” ambazo zilifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda, lakini tangu msanii Mozey Radio afariki dunia miaka mitatu iliyopita Washington amefeli kutoa ngoma kali.