Mafanikio ya album yake ya kwanza ya ‘Invasion of Privacy’ bado yanamtesa rapa Cardi B kutoka nchini Marekani.
Rapa huyo amesema mpaka sasa amesharekodi jumla ya nyimbo 50 lakini bado hajaridhika kwani anapata hofu na hajui ni ngoma zipi ziingie kwenye album yake ya pili.
Ikumbukwe sio mara ya kwanza kwa rapa Cardi B kukiri kuwa yupo chini ya shinikizo kwani mwishoni mwa mwaka wa 2020 alidai kuwa na hofu na angekosa kutoa wimbo mkali tena, watu wangesema ameshindwa na muziki.
Hata hivyo kinyume na hofu yake, mwezi Agosti mwaka huo aliachia mkwaju wake uitwao “WAP” aliomshirikiaha Megan Thee Stallion na mpaka sasa dunia inazungumza habari zake.