RITA ORA ALAZIMISHWA KUKAA KARANTINI NCHINI AUSTRALIA,MUDA MFUPI BAADA YA KUTUA.

You are currently viewing RITA ORA ALAZIMISHWA KUKAA KARANTINI NCHINI AUSTRALIA,MUDA MFUPI BAADA YA KUTUA.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki Rita Ora kutoka nchini Uingereza, amejikuta akilazimishwa kukaa karantini dakika chache tu  baada ya kuwasili Sydney, nchini Australia siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, ambao ndio umeripoti undani wa habari hiyo, ulinasa video inayomuonesha Rita Ora akisubiriwa na polisi baada ya kutua Uwanja wa ndege ambapo alisindikizwa na Polisi mpaka hotel ambayo alipaswa kufikia, huku akilazimishwa kukaaa karantini kwa wiki 2.

Imeripotiwa kwamba, Rita Ora hatoruhusiwa kutoka nje ya chumba cha hoteli aliyofikia mpaka siku 14 zitakapo kamilika na chakula atapelekewa na mtoa huduma maalumu katika chumba chake.

Rita Ora ametua nchini Australia kwa ajili ya kuungana na Keith Urban na Guy Sebastian katika paneli ya majaji ambao watahusika kwenye mashindano ya uimbaji.

Hata hivyo Serikali ya Australia imekosolewa vikali kutokana na kitendo cha kuruhusu watu maarufu kuingia nchini humo wakati watu zaidi ya elfu 40 wana maambukizi ya virusi vya corona.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa