Msanii wa muziki nchini Tanasha Donna amesisitiza kuwa yupo single ikiwa ni siku chache tangu akutane na mzazi mwenza Diamond Platinumz.
Akizungumza alipotua nchini kutoka Tanzania, Tanasha amesema hajerudiana na Diamond Platinumz kama wengi wanavyodhani ila wanasaidia na mkali huyo wa Bongofleva kutoa malezi kwa mtoto wao.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gere” amenyosha maelezo kuhusu video aliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha akimnong’onezea kitu Diamond Platinumz kwa kusema kuwa watu walitamsifiri vibaya video hiyo kwani hana mazoea ya kubusu au kuonyesha mahaba hadhari.
Ikumbukwe Tanasha Donna amekuwa nchini Tanzania kwa kipindi cha wiki moja iliyopita ambako alikuwa ameenda kwa ajili ya kumpeleka mtoto wake Naseeb Junior kumuona babake Diamond Platinumz lakini pia kufanikisha mchakato wa kuandaa video ya wimbo wake wa Nandy.