“WASANII WA UGANDA WANA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WANIGERIA, TUNAWAHITAJI KULIKO WANAVYOTUHITAJI” – SPICE DIANA.

You are currently viewing “WASANII WA UGANDA WANA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WANIGERIA, TUNAWAHITAJI KULIKO WANAVYOTUHITAJI” – SPICE DIANA.
  • Post category:Burudani

Staa wa muziki nchini uganda Spice Diana anaamini tasnia ya muziki nchini humo inahitaji raia wa nchini ya nigeria ili imarike zaidi.

Kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda Spice Diana amesema wanamuziki wa Nigeria wamejipanga zaidi na wanafanya muziki wenye viwango vya kimataifa ikilinganishwa na wanamuziki wa Uganda.

Aidha amesisitiza kuwa wasanii wa uganda  wana mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzao kutoka nigeria ili kuboresha na kujenga tasnia ya muziki nchini humo kwa faida ya  vizazi vijavyo.

Kauli ya spice diana inakuja mara baada ya kuulizwa ana maoni gani juu ya matamshi ya msanii Bebe Cool aliyedai kuwa wasanii wa nigeria wanahitaji sana raia wa uganda kwenye muziki wao kwani ndio wamekuwa mstari wa mbele kusikiliza kazi zao.

Ikumbukwe Bebe Cool na raia wa Nigeria waliingia kwenye ugomvi mara baada ya wasaani wao Omah Lay na Tems kukamatwa nchini Uganda kwa kukiuka kanuni za kuthibiti Corona, kitu ambacho kinadaiwa kuwa Bebe Cool ndiye alichochea kukamatwa kwa wasaani hao.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa